MADHARA YA UPOFU WA FIKRA
Tazama picha hapo chini kwa makini
👇
Madhara ya upofu wa fikra!
Umegundua nini katika picha hapo juu baada ya kuitazama kwa umakini?
Katika picha hii kuna vitu vya msingi vifuatavyo;
1) Farasi
2) Kamba iliyomfunga farasi
3) Kiti
4) mazingira jirani
Ufafanuzi wa picha
1) Je! Farasi ni nani?
Katika picha yetu, farasi ni mtu yeyote mwenye hofu ya kufanya jambo ambalo kwa macho yake ya kawaida analiona ni kubwa na gumu mno, tofauti na uhalisia wa hilo jambo.
Kwa maana laiti huyo farasi angefumbua macho na kukiona kinachomzuia, angekwisha ondoka mahali hapo haraka sana na kwenda kwenye malisho.
Watu kama huyu farasi muda mwingi huwa na hofu, hawajiamini, na hawana mawazo yanayozarisha au kujenga mambo makubwa (productive thoughts). Ushindi kwao ni kitu adimu sana, lakini kushindwa ndiyo sehemu kubwa ya maisha yao! Usiwe miongoni mwa farasi hawa.
2) Je! Kamba ni nini?
Kamba ile iliyomfungia farasi ni hofu (fear), kukosa kujiamini (lack of confidence), na upofu wa fikra (mind blindness). Ukiogopa kuthubutu kufanya jambo, hautalifanya. Usipojiamini kuthubutu kufanya jambo, hautalifanya na hata kama ukilifanya hautalifanya kwa kiwango kikubwa. Ubongo wako ukilala usingizi, pia utakuwa na mawazo duni na ya kushindwa, hivyo si ajabu kutokuona umuhimu wa kuthubutu na kufanya mambo kwa viwango vikubwa.
Je! Unadhani ni kamba gani imekufunga, inayokukwamisha kufika mahala unapohitajika kufika?
Fungua kamba uliyonayo.
3) Je! Kiti ni nini?
Kiti ni vitu au mambo madogo tunayohofia kuyakabiri kwa kuyaona ni makubwa na ni magumu sana kwa macho yetu ya kawaida, lakini kumbe sivyo yalivyo kabisa katika uhalisia wake!
Hebu tazama tena picha vizuri; je, unadhani kiti ambacho farasi amefungiwa kinaweza kumzuia kutoka alipo na kwenda kula majani katika mazingira jirani na kujikinga na jua?
Kwa akili ya haraka, jibu ni hapana!
Vivyo hivyo hata sisi tunaweza kuwa na mipango mikubwa ili kufikia ndoto zetu, lakini tunashindwa kuthubutu kuanza kupiga hatua kutokana na vitu vidogo tu vinavyotuzuia, na tunafikiri vina hatari kubwa au vigumu sana kumbe hapana! Tunazuiwa na vitu vidogo sana ambavyo tuna uwezo wa kuvikabiri na kuvishinda.
Je! Unadhani umefungwa au umekaa kwenye kiti cha aina gani kinachokuzuia kufanya mambo makubwa na kushindwa kuishi katika kusudi lako?

Comments
Post a Comment