Posts

Showing posts with the label makala

JINSI YA KUMWAMBIA MTU UNAMPENDA

 MIFANO 7 YA JINSI YA๐ŸŒน KUMWAMBIA MTU UNAMPENDA❤️๐Ÿ˜˜ KWA MARA YA KWANZA 1. Kwa Lugha ya Wazi na ya Dhati Njia ya wazi na ya moja kwa moja Toka nimeanza kukufahamu, maisha yangu yamebadilika na kuwa na furaha sana. Nataka ujuwe leo kuwa ๐ŸŒน❤️nakupenda kwa dhati na ningependa tuwe pamoja. 2. Kwa Kuonyesha Amani Anayokupa Njia ya kutumia hisia na amani ya ๐Ÿซถmoyo Uwepo wako kwenye maisha yangu unanipa amani ambayo sijawahi kuihisi mahali pengine popote. Moyo wangu umechagua kuwa wako, nakupenda sana. 3. Ujumbe Fupi wa Mahaba Njia ya fupi na yenye msisimko Siwezi kuendelea kuficha hisia zangu tena. Wewe ni mtu wa kipekee sana kwangu na nakupenda kutoka dimbwi la moyo wangu๐Ÿ’. 4. Kwa Lugha ya Kingereza Njia ya kiingereza (English Touch)    I have been holding these feelings for so long, but today I want you to know the truth. I love you๐Ÿ˜˜, and you mean the world to me. 5. Kwa Kutaja Thamani Yake Kwako Njia ya kumweleza jinsi anavyokuvutia. Kila siku inayopita inanifanya nigundue ...

JUMA NA SIMU YA MAMA

Juma alikuwa na tabia ya kutumia simu ya mama yake bila ruhusa. Mara nyingi mama yake alikuwa akikasirika na kupaza sauti, lakini siku moja aliamua kutumia njia tofauti. Alimuita Juma na kukaa naye sebuleni. Akamuuliza, “Unajua kwanini sipendi uchukue simu bila kuniambia?” Juma akajibu kwa sauti ya chini, “Nilitaka kucheza game tu.” Mama yake alimweleza kuwa kwenye simu kuna kazi muhimu na taarifa za familia. Kisha akamwambia, “Kuaminiana ni muhimu sana ndani ya familia.” Badala ya kumfokea, walikubaliana muda maalum wa Juma kutumia simu kwa ruhusa. Baada ya wiki chache, Juma alianza kuomba ruhusa kila mara kabla ya kutumia simu. Mama yake aligundua kuwa mazungumzo ya upole yalimbadilisha zaidi kuliko hasira. Funzo: Nidhamu yenye mazungumzo na kueleweshana humjenga mtoto mwenye uwajibikaji.

ZAWADI YA SARA

Sara alikuwa akipenda sana kucheza na vifaa vyake vya shule. Siku moja baba yake alimnunulia kalamu nzuri ya rangi ya bluu. Kesho yake alipofika shuleni alimkuta rafiki yake Neema hana kalamu kabisa. Neema alikaa kimya darasani kwa sababu aliogopa kuadhibiwa na mwalimu. Sara alimwangalia kwa huruma, akakumbuka jinsi mama yake alivyomfundisha kusaidia wengine. Bila kusita, alimpa Neema kalamu yake mpya. Aliporudi nyumbani alimweleza baba yake kilichotokea. Baba yake alitabasamu na kusema, “Mtu mwenye moyo wa kusaidia huwa tajiri wa upendo kuliko mwenye vitu vingi.” Kesho yake baba alimnunulia Sara kalamu nyingine na kumpongeza kwa moyo wake mzuri. Funzo: Watoto hujifunza upendo na kusaidia wengine wanapoona wazazi wakithamini matendo mema.

AMANI NA PESA YA SOKONI

 Amani alikuwa mtoto wa miaka 9 aliyependa sana kwenda sokoni na mama yake. Siku moja mama alimpa fedha kwenda kununua nyanya. Baada ya kununua, muuzaji alimrudishia chenji kubwa kuliko iliyotakiwa. Amani alifurahi kimya kimya na akafikiria angenunua pipi nyingi. Lakini aliporudi kwa mama yake, mama alimuuliza kwanini chenji ni nyingi hivyo. Amani alikaa kimya kwa muda, kisha akasema ukweli. Mama yake hakumpigia kelele wala kumpiga. Alimshika mkono na kusema, “Mtoto mwema si yule asiyekosea, bali anayekubali kusema ukweli.” Walirudi sokoni pamoja na kurudisha fedha ile. Muuzaji alimshukuru sana Amani na kusema, “Utakuwa mtu mwaminifu sana ukikua.” Kuanzia siku hiyo, Amani alianza kujivunia kusema ukweli hata pale inapokuwa ngumu.  Funzo: Kumfundisha mtoto kusema ukweli huanza kwa mazungumzo yenye upendo, si vitisho.

ANDALIO LA SOMO

  ANDALIO LA SOMO   Jina la Shule:                                                               Jina la Mwalimu:                                       Kidato:                                                            ...

MADHARA YA UPOFU WA FIKRA

Image
Tazama picha hapo chini kwa makini ๐Ÿ‘‡ Madhara ya upofu wa fikra! Umegundua nini katika picha hapo juu baada ya kuitazama kwa umakini? Katika picha hii kuna vitu vya msingi vifuatavyo; 1) Farasi 2) Kamba iliyomfunga farasi 3) Kiti 4) mazingira jirani Ufafanuzi wa picha 1) Je! Farasi ni nani? Katika picha yetu, farasi ni mtu yeyote mwenye hofu ya kufanya jambo ambalo kwa macho yake ya kawaida analiona ni kubwa na gumu mno, tofauti na uhalisia wa hilo jambo.  Kwa maana laiti huyo farasi angefumbua macho na kukiona kinachomzuia, angekwisha ondoka mahali hapo haraka sana na kwenda kwenye malisho. Watu kama huyu farasi muda mwingi huwa na hofu, hawajiamini, na hawana mawazo yanayozarisha au kujenga mambo makubwa (productive thoughts). Ushindi kwao ni kitu adimu sana, lakini kushindwa ndiyo sehemu kubwa ya maisha yao! Usiwe miongoni mwa farasi hawa. 2) Je! Kamba ni nini? Kamba ile iliyomfungia farasi ni hofu (fear), kukosa kujiamini (lack of confidence), na upofu wa fikra (mind blindness)...