JIULIZE MASWALI HAYA MUHIMU
Kabla ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi , jiulize maswali haya:
1.Je, yeye ni mke wako?
2.Unampenda kweli? Najua unapenda umbo lake ,kifua chake ,mwili wake ...lakini kwanini hujamuoa?
3.Baada ya kulala naye ,je utakuwa na ujasiri wa kumuoa?
-Je, bado utapenda tabasamu lake?
-kifua chake?
4. Kama akipata ujauzito ,utasema "ndiyo ,mimi ndiye mtunzi mwenye majivuno ?" Au utaachana nae ahangaike peke yake na ulimwengu ? Je utatoroka?
5. Kama atakupigia simu kukijulisha kuwa ni mjamzito ,utachagua nini ? Kulea mtoto au kutoa mimba. Na kama atakufa wakati wa kutoa mimba ?
6. Kama akijifungua , je utamhudumia yeye na mwanae? Je utaweza kufanya hivyo?
7. Fikiria ,mwanaume mwingine akimfanyie hivyo dada yako bila kumuoa.Je ,ungefurahi ? Jenga picha kichwani mwako ; mwanaume huyo akimpa ujauzito dada yako kisha kumterekeza.
8. Kama yeye ni mrembo kiasi kwamba unalala naye kila wakati, kwanini haitoshi kumfanya awe mke wako?
9. Kwanini hukumuoa kama mke na kufurahi naye kila wakati nyumbani kwako?
10.Kama ukilala naye na ukamterekeza ,fikiria uchungu atakaopitia ;Je nga picha akilini, kama angelikuwa dada yako au binti yako.
Uhusiano wa kimapenzi haupaswi kuwa tu sehemu ya furaha tunapojisikia kufanya hivyo,
bali ni tendo linalopaswa kufikiriwa kwa kina , linaloonesha ahadi ya uaminifu kwa Mungu na kwa yule umpendaye,
Ndiyo maana tendo la ndoa linapaswa kufanywa ndani ya ndoa pekee, sio kabla (Uasherati), wala si baada( Uzinzi)
Mungu awabariki sana.
Comments
Post a Comment